Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wanadaiwa kufanya sherehe baada ya kuhamishwa kwa Dk. Mwakyembe katika wizara hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TPA wanadaiwa kufanya sherehe kwa kuhamishwa kwa Dk.Mwakyembe katika wizara ya Uchukuzi na kwamba ujio wa Sitta itakuwa mteremko kwao kuendelea na vitendo vya wizi kama ilivyokuwa awali kwa madai waziri Sitta hataweza kuwathibiti kama ilivyokuwa kwa Mwakyembe.
Kwa upande wake upande wake waziri Sitta amesema kuwa amepata taarifa ya kufanyika kwa sherehe hiyo na kwamba amewaonya kwa kufanya hivyo kwani vicheko vyao vitakuwa kulio na kama walizani maji yamepowa wanajidanganya kwa kuwa maji sasa ndio kwanza yanachemka.
“Nimepata taarifa kwamba baadhi ya wafanyakazi wa Bandari walifanya sherehe baada ya kusikia Dk. Mwakyembe amehamishwa katika wizara hii ya Uchukuzi, kicheko chao kitakuwa kilio chao na kina mwisho, waliodhani maji yamepoa wanajidanganya kwa kuwa maji sasa ndiyo yamechemka” alisema Sitta.
No comments:
Post a Comment