Thursday, January 29, 2015

VIJANA WILAYANI LUDEWA KATIKA MKOA WA NJOMBE WATAKIWA KUSOMA FANI ZA KUJIAJIRI

Kutokana na changamoto ya ugumu wa maisha inayowakabili vijanawengi katika wilaya ya ludewa mkoani njombe baadhi ya vijana wameamua kujiendeleza katika elimu ya kujitegemea kwakusoma fani mbalimbali zinazo tolewa na baadhi ya shule wilayani hapa. Wakizungumza na mtandao huu hivi karibuni baadhi ya vijana wanaosoma masomo ya ufundi wa kujenga na ufundi seremala katika shule ya ufundi madunda iliyopo katika kijiji cha madunda kata ya mawengi wilayani hapa walisema kuwa wameamua kusoma masomo hayo kwakuwa wanajua kuwa yata wawezesha kujiajiri mara baada ya kuhitimu masomo yao. Waliongeza kuwa kuna baadhi ya vijana wenzao wapo mitaani na hawana kazi maalumu ya kufanya hivyo maisha yao yamekuwa magumu kutokana na wao kuto jishughulisha na kubaki kuilaumu serikali bila mafanikio. Aidha walisemakuwa hadi sasa wamefanikiwa kupata ujuzi wa kutengeneza baadhi ya vifaa kwa kutumia taaluma yao ya ufundi hivyo wanaamini kuwa watakuwa na uwezo mkubwa wa kujitegemea mara wawapo mitaani bila kujali msaada kutokam kwa wazazi wao. Kwaupandewake mwalimu mkuu wa shule ya msingi na ufundi mandunda mwalimu Betram Chaula alisema kuwa hadi sasa kuna wanafunzi wengi ambao wanauwezo wa hali ya juu katika fani ya ufundi hivyo anaamini kuwa watakuwa na uwezo mkubwa wa kujitegemea katika maisha yao.

No comments:

Post a Comment