KOPUNOVIC AWAAMBIA SIMBA YEYE SI MCHAWI, WAMVUMILIE

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema anahitaji nafasi ya kutengeneza kikosi chake. Kopunovic raia wa Serbia amesema yeye si mchawi kwamba kila kitu cha Simba kitabadilika ndani ya siku mbili. "Ukocha ni kitu kinachohitaji kufundisha leo, kesho na keshokutwa. Mambo yanatakiwa kurudiwa, mambo yanatakiwa kubadilishwa. "Hakuna kitu ambacho kinatakiwa kufanyika kwa siku chache kikafanikiwa. Lazima niwe wazi, nahitaji muda. "Nimesema kuanzia siku niliyofika, hivyo tafadhari watu wanivumilie," alisema Kopunovic. Raia huyo wa Serbia amesema ana uhakika kikosi chake kitakuwa moto wa kuotea mbali kama atapewa muda.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: