Thursday, December 4, 2014

ORODHA YA MAKUNDI YA AFCON 2015 HAYA HAPA

Timu 16 zilizofuzu kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 huko Equatorial Guinea zimepangwa katika makundi manne usiku huu katika hafla ya upangaji makundi iliyofanyika jijini Malabo ambako fainali hizo zitafanyika . Makundi hayo yanaonyesha kuwa timu mwenyeji Equatorial Guinea imepangwa kwenye kundi ambako itakuwa na timu za Burkina Faso , Gabon pamoja na Congo brazzavile . Timu namba moja barani Afrika ya Algeria imepangwa Kundi C na timu za Afrika Kusini , Senegal na Ghana.Kundi B limejumuisha timu za Zambia , Tunisia , Cape Verde na Congo Drc , . Kundi jingine ambalo ni kundi C lina timu za Ghana , Afrika Kusini, Senegal na Algeria huku Kundi D likiwa na timu za Ivory Coast, Guinea , Cameroon na Mali . Mabingwa wa Afcon 2013 Nigeria hawataweza kutetea ubingwa wao baada ya kushindwa kufuzu.Michuano hiyo ambayo awali ilikuwa ifanyike nchini Morocco kabla ya kuhamishiwa nchini Equatorial Guinea itafanyika kati ya Januari 15 na Februari 8 mwakani. Kundi A . Equatorial Guinea Gabon Burkina Faso Congo Brazzaville. Kundi B Zambia Tunisia Cape Verde Congo Drc Kundi C Ghana Afrika Kusini Senegal Algeria Kundi D. Ivory Coast Cameroon Guinea. Mali. Michuano hii itafanyika kwenye miji minne huko Equatorial Guinea ambako Kundi A litacheza mechi zake kwenye kituo cha kwanza ambacho kiko kwenye mji wa Bata , Kundi B litakuwa litakuwa huko Ebibeyin , Kundi C litachezea kwenye mji wa Mongomo na Kundi litakuwa kwenye mji mkuu wa Equatorial Guinea huko Malabo.

No comments:

Post a Comment