NJOMBE,,,, MBUGE wa jimbo la kalenga Gopdfrey Mgimwa ametumia zaidi ya Tsh milioni 42 kutekeleza ahadi mbali mbali zilizoachwa na marehemu babake Dr Wiliam Mgimwa. Mbunge Mgimwa amefananikiwa kutekeleza ahadi hizo ndani ya kipindi kifupi cha miezi miwili toka alipoapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo. Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malagosi kata la Lyamgungwe wakati wa kukabidhi ahadi ya bati 80 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katibu wa mbunge Mgimwa Bw Martine Simangwa alisema kuwa hadi sasa mbunge huyo amepata kutekeleza ahadi mbali mbali zilizoachwa na mbunge Dr Mgimwa kwa zaidi ya asilimia alimia 50 . Alisema kuwa utekelezaji wa ahadi hizo umefanyika kwa kipindi kifupi cha miezi miwili pekee toka alipoapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo na kuwa jitihada za kukamilisha utekelezaji wa ahadi hizo ambazo ziliachwa na marehemu Dr Mgimwa zinafanyika . Simangwa alisema kuwa miongoni wa ahadi zilizotwekelezwa ni pamoja na zile za kuviwezesha vikundi vya Vicoba fedha za kukuza mitaji yao , ahadi za saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ,zahanati na nyumba za watumishi wa idara mbali mbali ikiwemo ya elimu na afya katika baadhi ya maeneo . Hata hivyo alisema kuwa jitihada mbali mbali zinafanyika ili kuendelea kukamilisha utekelezaji wa ahadi hizo kabla ya mwaka 2015 kufika . "ndugu wananchi mbunge Godfrey Mgimwa amekuwa halali kila wakati amekuwa akilitazama jimbo la kalenga na kuona sehemu ya ahadi ambazo zilitolewa na mbunge aliyetangulia ...hivyo anawaombeni mzidi kuwa na imani kazi inafanyika"

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: