FILIKUNJOMBE KUSHEREKEA KRISMAS NA UMEME MWAMBAO WA ZIWA NYASA. MBUNGE wa jimbo la Ludewa Mkoani Njombe kupitia chama cha mapinduzi (ccm) Deo Filikunjombe amewahakikishia wananchi wanaoishi mwambao wa ziwa nyasa kuwa atasherehekea pamoja nao sikukuu za X-Mass na mwaka mpya kwa kutumia umeme. Filikunjombe aliyasema hayo jana alipokwenda kuzindua na kisha kushiriki nguvukazi ya kufyeka njia ya umeme, kuchimba mashimo na kusimika nguzo hizo kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Lupingu ambako mradi huo umeanza baada ya serikali kutoa jumla ya shilingi bilioni 1.2 kati ya shilingi b.1.3 zilizopangwa kukamilisha mradi huo. Akizungumza katika eneo la mradi Filikunjombe alisema tumeamua kufanya nguvu kazi hii kwa wananchi wa vijiji vitatu vya Nindi, Lupingi na Mtumbati kwa sababu kubwa mbili tumeshindwa kusubiri mpaka serikali itakapopata fedha za kutosha mradi ambazo shilingi bilioni 1.3 lakini fedha iliyopatikana ni bilioni 1.2 tu. nikaambiwa nisubiri fedha ikamilike ndipo nipewe kukamilisha mradi. ’’’jumla ya shilingi b.1.3 zilipangwa kukamilisha mradi huu wa umeme kutoka Ludewa hadi Lupingu lakini serikali ikapata bilioni 1.2 ni kutokana na hali hiyo nililazimika kuja kuzungumza na wananchi wangu ili tuchangie nguvu kwa kusafisha njia, kuchimba mashimo, kusimika nguzo na kuzisogeza.’’’ Wananchi walifurahia na kuunga mkono jitihada za serikali za kuleta umeme katika vijiji vilivyo pembezone mwa mwambao wa ziwa nyasa kwa kujitolea nguvu zao ili kuokoa jumla ya shilingi milioni 100 ambazo zingetolewa serikali kuwalipa vibarua. Hii ni nuru ya matumaini kama wananchi wangekataa na kusubiri serikali tungekuwa bado tunasubiri lakini kwa kuwa umeme ni wao na manufaa ni yao fedha zote zinztokz serikalini kupitia Tanesco. Kuhusu baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoshawishi wananchi wasishiriki wala kujihusisha na shughuli za maendeleo yao Filikunjombe aliwataka wanasiasa kuacha mawazo finyu na potofu serikali haiwezi kufanya kila kitu watumie vema ridhaa waliyopewa na wananchi. ‘’’nilipoingia madarakani nilikuta mradi mmoja tu wa umeme kila mwananchi mwenye macho anaweza kuona Ludewa tulikuwa nyuma, tumechelewa sasa tunakwenda mbele walau nuru ya matumaini inaonekana nashukuru rais kutuunga mkono barabara zinakwenda, miradi ya Liganga na Mchuchuma inaendelea.’’ aliongeza mbunge Aliongeza kuwa wakati anaingia madarakani alikuta kijiji kimoja tu katika vijiji 77 kikiwa na umeme lakini leo kuna vijiji 10 na sasa kuna mpango kabambe wa kupeleka umeme katika vijiji 49 vilivyopo katika kata za milimani na mwambao wa ziwa. Filikunjmbe amewataka viongozi kutengeneza mazingira mazuri ili kupunguza wimbi kubwa na vijana na wananchi kukimbilia mijini ambako kuna huduma nzuri Ludewa ni kubwa kuliko wilaya zote za mkoa wa njombe ina zaidi ya skwea mita 8000 lakini tuna watu wachache kuliko wilaya zingine ni kwa sababu ya vijana kukimbia.

ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: